Isaiah 44:22-24


22 aNimeyafuta makosa yako kama wingu,
dhambi zako kama ukungu wa asubuhi.
Nirudie mimi,
kwa kuwa nimekukomboa wewe.”


23 bEnyi mbingu, imbeni kwa furaha,
kwa maana Bwana amefanya jambo hili.
Ee vilindi vya dunia, piga kelele.
Enyi milima, pazeni sauti kwa nyimbo,
enyi misitu na miti yenu yote,
kwa maana Bwana amemkomboa Yakobo,
ameuonyesha utukufu wake katika Israeli.

Yerusalemu Kukaliwa


24 c“Hili ndilo asemalo Bwana,
Mkombozi wako, aliyekuumba tumboni:

“Mimi ni Bwana,
niliyeumba vitu vyote,
niliyezitanda mbingu peke yangu,
niliyeitandaza nchi mwenyewe,

Copyright information for SwhKC